Friday, October 05, 2007

Comments to Muite/Jirongo on Kass FM 05 Oct 2007

Araap Sang,
Ahsante tena kwa kuwa na mpango wa leo. Ningependa kumshukuru Mhe Muite kwa kukaa ngumu katika hicho chama cha safina hata wakati huu wote ambapo upepo wa vyama vingine vilitingiza sehemu anakotoka (Ford-Asili 2002 wakati Muite alikuwa Ford-Kenya na 2007 alipokaa kwenye Safina ila Narc ilikuwa inavuma). Ila sijashangaa kuwa anamuunga mkono Mzee Kibaki naye ni "young turk". Nimuulize Muite maswali mawili:
  1. Je kuwaunga mkono Mzee Kibaki na Moi kuna ambatanaje na msimamo wake wa uongozi mzuri ambao Kanu ya Moi ilikuwa haina?
  2. Mwaka wa 2002, Mzee Kibaki alichaguliwa kwa vyama vya mseto kuambatana na kile ambacho kiliitwa MOU. Baadaye watu fulani walimshauri afutilie mbali ile ngazi (hata akajaribu kuvivunja vyama vya mseto huo) na pia akawamwaga wale walioenda kila kona ya Kenya kumpigia debe ili achaguliwe ila alikuwa hospitalini. Swali langu kwanyi wawili, kila mmoja baada ya mwingine: Kibaki anaweza kuaminika tena kuhifadhi MOU ingine ama vipi?

Comment: Ikiwa kwa kweli Michael Cheluget ameachishwa kazi wakati huu, niwaambie watu wa PNU kuwa mambo yamepanuka na unga imemwagika!
Mimi wenu, 'Agent of change - Mwanaharakati wa mabadiliko'

1 comment:

Anonymous said...

kusoma blog nzima pretty mema

Search Nandi Kaburwo