Friday, September 28, 2007

Questions to Kimunya on Kass FM 28 Sep 2007

Araap Sang na wageni wetu Asalam Aleikum,
Wewe ni wetu! Hao watu uliowaleta inaonyesha sababu ya kuuliza swali langu la kwanza:

1. Kwenye hivi vyama vya kisiasa, je wanawake wapo wapi? Mbona ni ODM ya Kalonzo tu ambayo inajaribu kuweka akina mama kifua mbele? Hata hiyo PNU ilipotambulisha timu ya Mzee Kibaki, hapakuwa na akina mama asili mia 30 il hali alisema nafasi zote za kazi ziwe na kitengo cha 1:3 kwao, ama ilikuwa MOU ingine iliyovunjwa?

2. Swali langu la pili ni kwa Mhe. Kimunya: Je Wakenya walipoimba 2002 kwamba yote yawezekana Kenya hiyo tuliimba kwa lugha ya taifa (Kiswahili). Baadaye juzi mtu fulani alisema kule Busia kwamba yeye alimshauri Rais apuuze MOU ile iliyomuwezesha kuchaguliwa. Swali langu ni kwenye mseto huu wa PNU ambao sasa mumekiunda, kunao 'wazee' wangapi ambao wameambiwa waende kando kidogo tufuge mto kisha murudi kushauri juu ya hii MOU mpya ya PNU? Je, Kibaki anaweza kuaminika tena kwa kuweza kuweka ahadi na wanaoambatana naye?

3. Kwa dada wa ODM-K, mbona Kalonzo amesahau pa kuwinda na sasa anamrudishia risasi Raila il hali anataka KUOMBA kiti? Mwambie anaposema kuwa Raila ni project ya serikali ajue ni ukweli mtupu kwani SISI wapiga KURA wa Kenya NDIO Serikali na Raila ni PROJECT YETU!
Ni mimi wenu 'agenti wa mabadiliko'

No comments:

Search Nandi Kaburwo